MASOMO

                           KUHARIBU KAMBA ZINAZOSABABISHA MATESO

                                           

Kuna aina nyingi za kamba ambazo mimi binafsi nazijua. Kuna kamba za ujenzi, kutengenezea fito, kuanikia nguo, kuvutia magari, kufugia mizigo na aina nyingine ambazo wewe unazifahamu.
Katika ulimwengu wa roho kuna aina tatu (3) za kamba nazo ni Kamba za Mungu ambazo hutoka mbinguni, aina ya pili ni kamba za mwanadamu ambazo hutoka duniani, na ya tatu ni kamba za shetani ambazo hutoka kwa shetani mwenyewe.
Na vyanzo vya kamba hizi zote hutoka kwenye madhabau. Za Mungu hutoka kwenye madhabau ya Mungu ambazo hutoa kwa wanadamu ili wazitumie. Zile za shetani ndizo humpa nguvu shetani kuweza kuwakamata wanadamu vizuri kwa kupitia dhambi wazitendazo hapa duniani.
Kitabu cha Waamuzi 6:22 kinasema Gideoni akanona ya kuwa ni malaika wa Bwana; Gidioni akasema, Ole wangu, Ee Bwana Mungu! Kwa kuwa nimemowna Bwana uso kwa uso. Hata unatakiwa kama unataka kumuona Mungu uso kwa uso unachotakiwa kufanya kwanza ni kuvunja utaratibu wako ambao ulikuwa umeuzoea tangu hapo mwanzo na ndipo ujenge na Mungu.
Sasa naona tuangalie hizo madhabau ambazo humuumiza mwanadamu kwa njia moja au nyingine kupitia kwa shetani. Ziko saba nazo ni Madhabau ya dhambi, wasio haki, mauti, kuzimu, mateso, ukiwa, ubatili, nira, wanadamu, kupimia, na fedha.
Tuanze kuangalia madhabau ya dhambi ni kwa kamba za shetani hutumia kumvuta mtu kwa urahisi kutokana na dhambi anazotenda na akisha mvuta huyo mtu huanza kumfunga mafundo, mitego ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja ya afya ya mtu, fedha katika kufunga kipato chake, au hata katika biashara zake iwapo mtu huyo atakuwa ameangukia dhambini.
Nayo Mithali 5:22 inasema, Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. Je wewe kamba za dhambi zako au za wazazi wako  hazijakushika mwenyewe ndiyo maana unapatwa na mateso hayo yote. Unachotakiwa kufanya ni kufanya toba ya kweli ambayo itakuweka huru na kamba hiyo ya dhambi.
Ya pilini kamba za wasiohaki.  Tuone Zaburi 119:61 inasema; Kamba za wasio haki zimenifungako, Sikuisahau sheria yako.  Hapa wanazungumziwa wale ambao hupenda kuwakatisha wenzao tamaa wakati wa kumfuata Mungu. Huwapa maneno ya kebehi, kejeli na hata dharamu ya kuwa matatizo yote hayoi unayoyapata kama Mungu wako yupo si akuondolee. Lakini hawajui kuwa kama mtu anataka kumfuata Mungu lazima apitie kwenye mateso. Dhahabu haiwezi kuwa nzuri hadi ipitishwe kwenye moto.  Na kama ukikataa kupishwa kwenye mtoto utawezaje kung’aa?
Kamba za tatu ni za Mauti. Mauti hubeba nguvu ya kifo, pia hupoteza kabisa uhai wa kila kitu ikifanyacho lazima kife. Ikiwa mtu ameanzisha biashara huanza vizuri lakini mwisho wake huishia kufilisika kwa biashara yako. Pia katika kazi unaweza ukafanya kazi zako vizuri lakini kabla umri wako wa kustaafu haujafika unaweza ukaipoteza hiyo kazi na ukaendelea hivyo maisha yako yote.
Vile vile, inaweza kuathiri katika uzao, kama mtu anakuwa ana kipawa cha kitu Fulani ambacho mara nyingi akifanya jambo fulani watu hushangazwa na hicho kipwa lakini inatokea tu ghafla kipawa hicho kinapotea au kuzimika kama mshumaa unavyozimika ukiwekwa kwenye upepo.
Zaburi 18:4 inasema, Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za mauti hizo huweza kusababishwa na magonjwa, hofu, njaa, woga, kutafuta mali kwa njia zisizo halali na vitu vingine vingi.
Aina nyingine ya nne ni Kamba za kuzimu. Zaburi 18:5  inasema, Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili. Hapa tunaona jinsi kamba za kuzimu zinavyoshirikiana karibu sana na kamba za mauti ili kamba za mauti ikisha mmeza mtu humpa kwenzake kamba za kuzimu kumalizia kazi zake. Hivyo unaona jinsi shetani alivyopanga watu wake kwa ushirikiano mkubwa kuwadhuru wanadamu.
Angalia jinsi Isaya 14:9 inasema; Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokula; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi. Hapa tunaona kuwa mtu asiye haki anapokufa kuzimu hutaaruki ikimpokea kwa shangwe kwa mwenzao amefika je wewe unataka nayo kuzimu itaaruki kwa kufa na dhambi zako unazozikumbatia? Muda bado fanya toba kweli.
Kamba za tano ni za Mateso. Ayubu 36:8  inasema, Nao wakifungwa kwa pingu, Wakitwaliwa kwa kamba za mateso; watu wengi hapa ndipo walipokuwa wamenaswa na kamba hii ya mateso kuanzia jua linapochomoza hadi pale linapozama ni mateso mtindo mmoja hakua ahueni hata kidogo. Dalili za kamba hiii ya mateso ni utamuona mtu wa aina hiyo hana raha katika maisha yake anayoishi, kazini anapofanya kazi, majirani zake wanaomzunguka  na hata kwenye familia yake ni vurugu mtindo mmoja.
Hizi kamba za mateso zina vitu saba (7). Tuone Ayubu 5:16-27 lakini tuone ule mstari wa Ayubu 5:19 unasema, Yeye atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapanba uovu utakaokugusa. Katika kamba hizi ambazo zinakuandama katika maisha yako Bwana anauwezo kwa kukuokoa katika vitu hivyo saba.
Cha kwanza ni kukuokoa katika kamba za mauti na njaa. Unaweza kuzongwa na njaa kwa muda mrefu ambapo kama njaa ikiwa ni kali kupita kiasi huweza kusababisha mtu kupoteza maisha Mungu anaweza akakukuepusha na baa hilo la njaa lisikupate likaishia njiani.
Kitu cha pili wanakuokoa na nguvu za upanga, wa tatu ni mapigo ya ulimi, wan ne ni aina zozote za maangamizo ambayo unayajua yanaweza kukudhuru kwa njia moja au nyingine uhai, afya, uchumi wako na vitu vingine vingine. Pia vitu kingine cha tano ni huponjwa na wanyama wakali, cha sita huponywa na laana ya uchache pia cha saba ni vifo vya mapema.
Kamba ya sita ni kamba za Ukimwa. Hapa asilimia kubwa huwapata wale watu wandoa ambao kati ya mwenza mmoja ameendea kwa mganga na kufanyiwa dawa huko ya kupendwa zaidi. Hapa utaona kuwa mwanaume au mwanamke akiingia ngani huona kama vile ameingia chooni anaona kuwa hapafai kukaa ingawa ni nyumbani kwake.
Lakini anapotoka nje hujioni kuwa afadhali ya kukaa nje kuliko kukaa ndani. Isaya 34:11 inasema, Kaati ya nungu wataimiliki, bundi na kunguru watakaa huko, naye atanyosha juu yake kamba ya ukiwa na timanzi ya utupu.
Kamba ya saba ni Kamba za Ubatili Isaya 5:18 inasema, Ole wao wavutao uovu kwa kamba za ubatili, na dhambi kama kwa kamba za gari!  hapa inawapa onyo wale wanaovuta sigara ana aina nyingine yeyote ya kileo hicho. Kwamba yeyote anayevuta sigara na aina yeyote ya kileo hicho huvuta uovu.
Kamba ya nane ni Kamba za Nira. Isaya 58:6, inasema, Je, saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Mfano wa kamba hizi ni kwa wale ambao wakulia wanautumia au kama si mkulima umeshawahi kuona jinsi ng’ombe wanaofanya kazi ya kulima hufungwa nira kwenye shingo zao. Hapa tunaona kama hizo nira za hao ng’ombe zisipofungwa vizuri hawataweza kulima.
Tunoana katika 2 Wakorinto 6:14 inatuonya kuwa tusifungiwe nira na wale wasioamini sawasawa na kuenenda na marafiki ambao ni wevi, wanzinzi, washerati, waongo, wachawi na wangine wengi ambao ni machukizo mbele za Mungu, hatuwezi kuchanganya nuru na gizi kwa sababu panapo nuru giza haikai.
Kamba ya tisa ni Kamba za Mwanadamu; Hosea 11:4 inasema, naliwavuta kwa kamba za kibinadamu, kwa mafungo ya upendo; nami nalikuwa kwao kama hao waondoao kongwa tayani mwao, nikaandika chakula mbele yao.
Hizi kamba za wanadamu humsababishia mtu kumwa mwoga na hata kama ulikuwa mtu ulimpa kitu kwa kutimia mikono yako kwa hiari yako mwenyewe kwa moyo safi lakini mtu yule uliyempa kile kitu akaenda akanda kwa mganga au kama ana yale maarifa ya kishetani anaenda kwenye kaburi na kuzika kile kitu ulichompa kwa mikono yako mwenyewe kwa hiyo atakuwa amekufunga kila kitu katika maisha yako. Hutaweza kufanikiwa katika jambo lolote maana kaburi halisemi na vitu vyako vyote utakavyofanya kuanzia hapo havitafanikiwa.
Kamba ya kumi ni Kamba za Kipimo. Hizi kamba ambazo mtu anakuchokoza kwa njia yeyote ile ili ufanye uovu. Hapa hutumia njia nyingi anaweza kukujaribu katika uwezo wako kazini, kujitoa kwako katika kazi za Mungu na hata za kijamii. Atakupa jambo ulifanye ukifanikiwa hukasirika la usipofanikiwa hapo ndipo huanza kuivuta hiyo kamba yako ya kipimo kwa lile kosa ulilofanya kwa wakati ule. Unatakiwa kujiangalia sana kwa huyo mtu uliyekuwa naye karibu je, nirafiki wa kweli au ni kamba ya kipimo chao?
Kamba kumi na mmoja ni kamba za Fedha; hapa kuna zile kamba za chuma ulete ambapo kila hela unayopata kutokana na kazi unayofanya hufanyii kazi yeyote huisha tu bila kufanya kitu cha maana. Unaweza ukatumia katika anasa na uchawi, uganga, matambiko, makafara, kutoa mimba, na vitu vingine vingi ambavyo utatumia fedha yako. Mhubiri 12:6 inasema, Kabla haijakatika kamba ya fedha, au kuvunjwa bakuli la dhahabu; Au mtungi kuvunjika kisimani; Au gurudumu kuvunjika birikani.  Tunakumbushwa kuwa je kamba zetu za fedha tumeziunganisha wapi wa waganga, madhabau gani, matambiko, ulevi, uzinzi, uasherati, anasa, uuaji na vitu vingine vingi.
Watu wengi hujilaumu kuwa nilikuwa na fedha nyingi lakini sasa sina je, hujiulizi kamba yako ya fedha aliyokupa Mungu umeiunganisha wapi? Ukisha kumbuka kuwa umeiunganisha sio mahali pake, hujachelewa unatakiwa kuomba Mungu toba ya kweli na kurejeza kamba yako ya fedha.
Jinsi ya kuharibu hizo kamba zote 11 nilizozitaja hapo juu. Unachotakiwa kuzingatia kwanza ni kufanya maombi ya vita Waefeso 6:10. Tumia malaika, damu ya Yesu, Maneno ya kinabii, Uwe mtu wa imani, tumia malaika kwa upanga ukatao kuwili. Kumbuka kabla ya kuanza maombi hayo ya vita jikague kwanza wewe ukoje uko safi au una mawaa? Na kama una mawaa huri magotini uombe toba ya kweli ili upate kibali cha kukata hizo kamba kumi na moja.

                                                                  


                               KUREJEZA NGUVU ZA UJANA ZILIZOPOTEA
Mara nyingi mtoto anapozaliwa huwa kunafuraha sana katika ile familia ambayo wamepata mtoto. Pia ndugu jamaa na marafiki kutoka sehemu mbalimbali huja kumuona mtoto aliyezaliwa wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali, hali kila mmoja hawezi kuja kwa mtoto akiwa mikono mitupu.
Pia uzee nao hufurahiwa sana kwa kuwa mtu huyo huwa na busara na hekimka za kutoa ushauri mbalimbali. Lakini umri wa vijana wengi huwa na maisha yenye uchungu ambapo mwisho wake huishia kubaya. Lakini yupo mmoja awezae kurejeza ujana wako.
Tuone anasemaje, Zaburi 103:4-5. Auokomboa uhai wako na kaburi. Aushibisha mema uzee wako, ujana wako ukarejezwa kama tai.  Je, wewe kijana ujana wako umeupotezea wapi? Mpaka hivi sasa unasumbuka kwa mateso ambayo yanakuandama siku hadi siku, hadi umekata tamaa ya maisha ya ujana wako?
Tuangalie huyu ndege tai ambaye akiona kuwa amekuwa mzee huenda sehemu ya mbali sana kwenye pango ambapo hujificha huko huku akinyonyoa manyoya yake ya mwili mzima. Hapo huanza kuota manyoya mengine mapya na yakisha kamilika yote hutoka kwenye lile pango na kuanza maisha mengine upya.
Je, wewe umeisha ingia pangoni kuweza kunyonyoa hayo manyoya yako ambayo yaliyokufanya upoteze uhai wa ujana wako? Hujachelewa Yesu anakusubiri uje pangoni ili aweze kukukarabati ili ukitoka uwe mpya katika ulimwengu huu.
Wengi wetu tuliuza ujana wetu kwa waganga, uchawi, uasherati, uzinzi, maangano, matambiko, ibada za sanamu, ulevi, wizi, uongo na vitu vingine vingi ambayo havimpendezi Mungu.  Hivi vyote vilivyopoteza ujana wako ni vitu ambavyo shetani alikutenda kwa hili ili uwe mfuasi wake.
Hujachelewa unachotakiwa kufanya ni kudai miaka yako kwa muumba wako ambaye ni Baba yetu wa Mbinguni; ila tusisahau kuwa Mungu wetu ana kanuni zake ambazo yeye husimamia kwenye kweli, haki na hukumu.
Je, sisi tu wa kweli mbele za Mungu na ndugu zetu au tunampenda Mungu tusiyemuona na kumchukia ndugu ambaye tupo naye.  Tuone Yoeli 2:21-26. Lakini hapa tuangalie zaidi ule mstari wa Yoeli 3:25,26 unasema: Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililolituma kati yenu. Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Tujiulize, ni kwa nini mtu huanza na maisha mazuri na kisha mwisho wa maisha yake huishia maisha ya tabu na dhiki kuu? Ni nini kinachosababisha mtu kuwa na maisha ya aina hii. Pia Mungu husababisha mtu kupatwa na matatizo hayo kwa sababu mara nyingi mtu anapopata neema na utajiri huwa wanamsahau aliyewapa na huanza kuenda kwenye miungu mingine ambayo ni chukizo mbele zake yeye aliyekupa.
Na hapo shetani huwa na ushawishi mkubwa wa kuwahadaa wana wa Mungu kwa hila ambazo hutumia ikiwa nia pamoja na hucheza na afya, uchumi, elimu, ufahamu, nyota, uzao na vitu vingine vingi ambayo anajua hapo akigusa tu, huyu mwanadamu lazima atakengeuka na kuenda upande mwingine na hapo ndipo yeye huanza kuwinda nyendo za mwanadamu usiku na mchana na akisha mpata hapo kunakuwa hakuna tena amani katika familia, kazini, shuleni na hata sehemu yeyote ile ambayo upo.
Asilimia kubwa ya nguvu za ujana zimepotea sana kwenye makaburi. Utaniuliza ni kwa nini? Na mimi pia napenda nikuulize je, ulishaweza kwenda kwa mganga, ulishawashi kutambika, ulishamsindikiza rafiki au jamaa yako kwenda kutoa mimba, ulishirikia sadaka za mizimu, ulifanya maagano ya ushirikiana wa aina yeyote ile au mila na desturi ambazo umerithi kutoka kwa wazee wako?
Tuangalie hivi vichache, tuanze kuangalia kuhusu maagano. Je, ulishawahi kufanya maagano yeyote, ukiwa ni wewe kama wewe au na ndugu, jamaa, rafiki, Mungu na hata shetani?
Je, ulishawahi kwenda makaburini kufanya dawa, ulitumwa na mganga, ulichanjwa chale makaburini, ulienda kumsindikiza rafiki  yako.
Tuone 2 Wafalme 1-17 lakini hapa tuangalie zaidi 2 Wafalme 17-18 inasema; wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. Kwa hiyo akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake, wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake.
Je, wazazi wako walishawahi kukupeleka kwa waganga, au mimba yako ulipatikana kwa mganga? Na wakati ulipozaliwa walienda kwa mganga, mila, matambiko, mizimu kwenda kukukabidhi wa wakuu wa pale?
Pia, walifanya machukizo hayo ambayo kwenye 2 Wafalme 17-18 Mungu anachukizwa nayo walienda kukufanyia wakiti ukiwa mdogo? Na kama hivyo vyote ulishawahi kupitishwa huko, tunaona kuwa ndio vyanzo ya kuliwa kwa ujana wako.
Katika Isaya 47:1-15 inasema; simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaambisha na tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda. Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.
Kuhusu mizimu wengi wetu tumejikuta kumeingia kwenye mtego wa shetani kwa kushiriki kuabudu mizimu kwa kutokujua au kwa kujua. Ikiwa ni pamoja na kushiriki ana kwa ana, kuchangia kwa hali yeyote ila ikiwa ni pamoja na fedha taslimu, vifaa vyovyote vilivyokuwa vikitumika katika kufanyia sadaka hiyo.
Mila nazo zimetufunga kutokana na kurithi kuto kwa wazee wetu yaani bila mtu kufanyiwa mila maisha yako hayawezi kwenda ndivyo tulivyokuwa tukiamini, na unaweza ukasongwa na nuksi, balaa na mikosi haya yote ndio inayoweza kwa namna moja au nyingine kuharibu nguvu ya ujana wako.
Hapa tunaona kuwa tunaonywa kwa tegemea nguvu za ibilisi badala ya kumtegemea Mungu anayekupa uhai. Je, tangu uivyotumia uchawi, uganga, matambiko, mila, ibada za sanamu una nafuu yeyote katika hayo matatizo yanayo kukabili? Au unasema afadhali ya jana kuliko leo.
Utawezaje kurejesha nguvu ya ujana wako uliopotea. Unachotakiwa kufanya ni kufanya toba ya kweli yaani ni kumaanisha kuwa unaikana nafsi yako ya kumwachia Mungu atende.
Kuhusu hadithi ya mwana mpotevua ambaye alidai mali kwa baba yake na alipopewa alienda kutapanya mali hiyo na makahaba Luka 15: 11-32. Lakini alipoona kuna maisha ya kule ni magumu siku hadi siku alisema moyoni, ni watumishi wangapi wa baba yangu wanakula na kusasa nami nataabika hapa.
Akakata shauri ya kurejea nyumbani kwa baba yake na baba alipomuona alifurahi hakukasirika maana mwanae aliepotea amerudi alimvika vazi, pete na viatu.  Sasa hata wewe umrudia Muumba wako leo hii ili upate kuvika vazi, pete na viatu.
Unatakiwa pia kufufua nguvu ya maombi ambayo hata kama hujawahi kufanya, lakini kuna roho ambaye wakati wote yeye yupo ukimtumia ipasavyo anauwezo wa kukufundisha maombi.
Pia tunatakiwa kujisahehe wenyewe. Imezoeleka mara nyingi kuwa lazima tuwasamehe wenzetu waliotukosea lakini tunajisahau sisi wewenye kujisamehe, na kama usipojisamehe wewe mwenyewe nani atakaye kusameme ikiwa imejikosea wewe mwenyewe?
Hapo ndipo utaweza kurejeza ujana wako uliopotea kwa toba, rehema, na msamaha. Hujachelewa anza sasa maana leo ni ya kwako kesho hujui ni ya nini?

NGUVU ULIOKUWA NAYO KATIKA KUMFUATA MUNGU
Imani, utii, Roho Mtakatifu.
Chanzo cha imani ni kusikia. Unatakiwa uwe makini kusikia ndipo utende uliolisikia. Na ikiwa kama husikii vizuri na ukatenda hicho ulichokisikia ambacho si sahihi kinaweza kukusababishia matatizo ambayo yataweza kukugharimu maisha yako yote.
Chanzo cha utii ni upendo bila upendo utii hauna nafasi katika maisha ya mwanadamu. Mungu alimuumba mwanadamu ili amtii, kwa sababu Mungu wetu ni mwenye wivu kwa sababu ya upendo alionao kwetu sisi wanadamu.  Adamu alivyokula tunda la mti wa katikati  ndani ya bustani ile, lakini kwa muda mchache tu alipoteza ule utii waliokuwa nao kwa kufanya kile ambacho waliambiwa wasikifanye. Mwanzo 3:1
Upendo wa Mungu ulionao kwetu sisi wanadamu ni mkubwa ambao hakuna mtu yeyete atakayeza kuufanya katika ulimwengu huu tulionao hivi sasa. Yeye alimtoa mwana wake wa pekee ili afe msalabali kwa ajili ya dhambi zetu. Je wewe unaweza kuutoa uhai wako kwa ajili ya ndugu yako?
Mungu ndiye aliyetoa maagizo elekezi kwa mwanadamu ya utii kwa maneno yale ya kutokula tunda  lile la mti wa katikati. Walipokosa utii kwa kumsikiliza shetani walivunja upendo na Mungu pale pale.
Ukitaka kuwa mtii ni lazima ufanye kile ambacho umeagizwa na kiongozi au mkubwa wako yeyote. Iwapo ukifanya kinyume cha hivyo ujue kuwa umeshatenda dhambi ya kukusudia au yakuto kukusudia. Na bila kufanya toba ya aina yeyote ila unakuja mbele za Bwana na shida zako ulizonazo kuanza kulalamika kuwa mbona hakujibu maombi yako. Wakati umeshasahau kuwa umemkosea hapo awali. Huko ni kumekosa utii mbele zake ukaenenda na njia zako.
Ni kitu Mungu amekitengeneza ili tukiri ile imani ya kumtumikia, utii  ndio huonyesha na kukomaza imani yako. Kwa mfano mtoto nyumbani anapokuwa mtii hupata ziada zaidi ya mwengine. Utii ni kitu cha lazima katika maisha ya mwanadamu.
Utii ni fimbo, ni upanga ukatao kuwili. Iwapo ukimuheshimu na kumtii mzazi wako yeyote atakupa kile utakacho, si kwa sababu u mzuri kuliko wengine bali ni kwa utii ulionao na unyenyekevu unaomfanyia kutoka moyoni mwako.
Lazima utii mamlaka tulionao. Kiongozi anapoagiza lazima kila mtu afuate agizo analotoa. Unatakiwa kuchagua kumtumikia Mungu au kumtumikia mwanadamu. Kazi ya bwana inatakiwa ipewe kipaumbele ndipo zile nyingine zifuate.  Hivyo vyote vitafanyika iwapo kuna utii ndani yake.
Utii una kanuni yake kubali kupokea ushauri, kubali kufundishika, kukemewa, kushutumiwa na hata kutukanwa, wazazi, majirani. Unapopokea ushauri unatakiwa uwe na moyo wa unyenyekevu. Unapaswa kutenda uliyoagizwa na si kwa mapenzi yako wewe.
Kubali kufundishika. Kizazi hiki kinapenda kulaumu watoto wao mwa matendo yao maofu wanayofanya. Wewe kama mzazi au mlezi umekaa na mtoto wako ukamfundisha kuwa, dunia ya sasa tunatakiwa tuenende hivi na sio hivi. Au tunamwachia mwalimu ndiye amfundishe? Au umemuacha ajifunze yeye mwenyewe. Jamii ya sasa hivi ina ukaidi wa kutaka kufundisha vitu hujiona kuwa kila kitu mtu anakijua, kumbe tu vipofu mbele za Mungu.
Ulimwengu wa sasa watu wengu hudhulumiwa haki zao kwa kutokana na unyonge waliokuwa nao. Ikiwa inaona hapa haki yangu imedhulumiwa na kila njia ya haki umetumia bila mafanikio yoyote yale. Usikate tamaa njoo mbele za Bwana umlilie, kumbuka Mungu wetu ni mkuu kuliko huyo anayekudhulumu haki zako. Muhubiri 5:8
Waebrania 12:5-8 ukikemewa naye kupitia matendo yako ukikaidi kutokana na kiburi chako hapo utakuwa hauna utii. Viongozi wawe wakali katika kanisa katika kukemea mambo yasiyompendeza Mungu. Baadhi yao wanaogopa wakiwakemea waamini wao wanaweza wakaogope. Je, hapo utakuwa unamtii Mungu au unatii mamlaka ya mwanadamu?
Utii ni silaha ya vita zote duniani. Mwanadamu hapo ulipo uko kwenye vita kila dakika. Kumbuka kuwa Mungu hupitia kwa mwanadamu na shetani pia hupiti kwa mwanadamu. Ni utii peke yake ndio utakaokusaidia kushinda vita hizo.
Vita hizo ni kati ya mwanamke wa shetani uwanja wa vita ni bustani ya Edeni. Edeni ni kila mahali ulipo wewe mwanadamu. Hii ni vita pekee ndio shetani aliyoishinda hapa duniani. Vita hiyo ilizidi kuwa ngumu pale Mungu alipoweka uadui katika ya Mwanadamu ya Mungu. Mungu alivyoona shetani amezidi lakini Mungu alileta uadui kati ya nyoka na mwanadamu. Ndipo shetani alishindwa kwa Yesu kufa pale msalabani kwa ajili ya dhambi walizotenda wanadamu.
Mama apatapo mimba humchukia mumewe kwa sababu kuna mwanya ambao shetani ameingia ndani hapo. Mtoto huchukua tabia zile za kale ambazo sheetani aliwahi pindi mtoto alipotungwa mimba.
 Shetani hufuatilia mimba ya mwanamke tangu siku ile apatapo mimba. Ndipo watoto wengi wazaliwapo huwa na tabia tofauti kwa sababu ya shetani kuingilia ujauzito ule. Na watoto kuwa na tabia tofauti katika nyumba moja.  Tumekombolewa kwa utii wa yesu pale msalabani kwa kuangikwa kwake.
Vita nyingine ni uasi na utii uwanja wa vita ni Kaini na Abeli. Iliacha kudaiwa baada ya Yesu kuangikwa pake msalabani. Kwa damu ya Yesu kumwagika pale Kalvari.
Vita nyingine ni ya uovu na wema. Uwanja wa vita ni duniani. Sodoma na Gomora. Ndoa za jinsia moja baadhi ya nchi huidhinisha kwenye katiba zao. Unatakiwa kujiepusha na hayo yote kwa kuwa utii mbele za Bwana tu.
Macho yako huangalia nini? Wengi wetu hupenda kuandalia vitu ambavyo ukisha fanya mazoea ya kuangalia vitu hivyo unaweza ikakusababishia kuuondoa uwepo wa Mungu katika macho yako na hivyo ukachafua hekalu la Mungu ambalo ni mwili wako kwa kuangalia kwa macho, kisha ukapatwa na tamaa ya mwili ukaangukia dhambini. Kataa mchezo wa kunajisi macho yako. Omba rehema kwa dhambi ambazo huzijui.
Kuna watu walishatolewa pepo kutokana na kuangalia luninga. Na ikiwa huamini hivyo kuwa shetani anaweza akamuingia mtu kutoka kwenye luninga anayoiangalia. Iwapo  mtumishi akasema kuwa weka mkono kwenye radio na ukapona. Je, wewe unayeangalia luninga usishangae vitu vya shetani vitakupata wewe moja kwa moja. Je, utamsingizia nani aliyekufanyia hivyo. Je si, wewe uliyejitakia yote hayo kwa tamaa zako za mwili.
Watu wengi huogopa kuwakosoa watu walio karibu nao kwa kuogopa kuchukiwa iwapo atamwambia ukweli. Usikasirike kumkosoa mwenzio hata kama atakuchukia ni heri uiokoe roho yake kuliko kuiacha iangamie.
Kwa kila jambo tufanyalo hapa duniani tunatakiwa tumshukuru Mungu kwa yote. Tukumbuke tunapomshukuru Mungu kwa kila jambo, ili imani yetu ihubiriwe ulimwenguni kote. Warumi 1:8
Vita ya Imani potofu imani na imani ya kweli, uwanja wa vita Red Sea. Vita hivyo ilipiganwa kati ya Mungu na Shetani kupitia wana wa Israeli,ndipo Farao na jeshi lake waliishia Red Sea (Bahari nyekundu). Wewe pia una Bahari nyekundu katika maisha yote ya kila siku, je uwatezaje kuvuka katika bahari hiyo ni kwa kuwa mtii  kusikia, mnyenyekevu na upendo.
Vita nyingine ni kati ya Kiza na  wana wa Mungu, uwanja wa vita inapopiganwa ni Duniani. Jinsi ya kushinda vita hiyo ni kuwa mtii kwa kuliitia jina la Yesu kila iitwapo leo.
Vita nyhingine  ni kati ya Manabii wa kweli na uongo. Utajuaje kuwa huyu ni nabii wa ukweli na huyu ni nabii wa uongo. Kwa kumtumia Roho Mtakatifu utaweza kusikia sauti ya ambayo itakuonyesha kuwa nabii huyu ni nabii wa kweli. Elia alishinda hiyo vita kwa uwanja wa Kalmeli. Nabii wa kweli huwa hana watu wengi, tukumbuke kuwa  njia ile ni nyembamba iendayo uzimani. Watu wengi hufuata manaabii wa uongo kwa kukosa maarifa ya Kiungu. Tumia macho, masiko
Vita ni kati ya Mikaeli na Lusifa vita hii inapiganwa kati ya Jeshi la Bwana na Jeshi la Uovu. Isaya 14:12:15. Katika vita inayokukabili katika maisha yako usipigane mwewe mwenyewe mtumie Malaika Mikaeli akupe upanga wake ili upigane vita hivyo.
Vita nyingine ni kati ya toba na dhambi, uwanja unaopiganwa vita hivyo ni duniani. Watu hawataki kutubu dhambi zao. Tena hujifanya hawazijui kwa makasudi kwa kuogopa kuzitamka mbele ya makuhani.  Kwa kukosa utii shetani hukufunika kwa kutokusema hizo dhambi zako. Kwa nini unaogopa kusitamka dhambi hizo, mbona kuna mitume ambao walifanya dhambi hapo awali lakini walipo tubu tu walikuwa huru na sasa wanaitwa watakatifu huko mbinguni?
Vita nyingine ni kati ya Nuru na Giza. Bustani ya Edeni, vita hivyo vilipiganiwa jagwani Mungu ndiye aliyeingilia kati. Jangwani alitoa nguzo ya moto ili kuongoza wana wa Israeli ni alama ya kuwaongoza. Kinyume cha utii watu waliiba vinyago vya waisraeli wakashindwa walipovichoma moto walishinda vita hivyo.
Watu wengu hutaka vitu vya gizani kuliko vya nuru. Iwapo utakuwa na subira mbele za Mungu atakupa vitu ambavyo shetani alivificha gizani, yeye Mungu atakupa vyote vya gizani.
Vita nyingieni ni ya Mwili na Roho, vita hivyo hupiganwa mwilini. Wagalatia 5:17 usiendekeza mwili wako kwa uchafu wa aina yeyote ile hilo ni hekalu la Bwana. Kumbuka unapochafua mwili wako unamfukuza Roho Mtakatifu awe mbali nawe kwa hivyo utabaki wewe peke yako kama kopo tupu. Majambazi wanaiba na kuua ni vita ya mwili na roho. Mume na mke kwa sababu ya mali ni vita vya mwili na roho.
Ipe nafasi roho itawale. Achana na habari ya mwili. Iwapo utafanikiwa kushinda utapata hitimisho ya roho yako.
Vita nyingine ni kati ya Mali na Mungu.  Mungu alitupa hapa duniani kumiliki, watu wangi huabudu mali kuliko Mungu. Viongozi wengi wa dini wanakusanya mali kutoka kwa waamini na kuua nguvu za waamini kushiriki kikamilifu katika kumtumikia muumba wao.
Fedha na dhahabu ni mali yake. Wewe unayeifanya kuwa ni yako umeitoa wapi. Ikiwa yeye anakupa kisha wewe hutaki kumtolea, ndio maana leo una mali nyingi lakini kesho huna kwa sababu hukuacha wewe kwa kuto kumrudishia kile alichokupa ukakipoteza kwa njia za uovu, yeye huenda kuwapa watu wake wanaomtii na kumheshimu.
Mahali pa juu na chini uwanja wa vita ni kichwani kwako. Elimu ya Mungu  Efeso 6:10. Tumia elimu ya mungu kuondoa elimu upotoshayo, udanganyayo,
Watu wa Mungu giza uwanja wa giza mwenyewe. Ili maisha yako yaweze kuwa mazuri unatakiwa ushinde vita ya upendo. Mahali penye upendo pana amani, haki, utulivu, uzalishaji wa kutosha, utele wa chakula, nyumba, magari chanzo cha yote ni upendo. Na kama huna upendo ni bure kabisa. Huwezi kumpenda mtu kama hauna utii. Utii
Vita nyingine ni Ubongo na elimu ya Mungu, uwanja uaopiganiwa vita hivyo ni masuala ya ibada hupiganwa na pale unapopungukiwa na hekima huwa na kujionyesha (showoff). Ubongo wake hupambana na ubongo wa Mungu.
Ukiwa na utii huwa na imani ya Mungu ambayo hutengeneza nguvu ya kumshinda ibilisi. Utii huanzia kwako mwenyewe. Hujitii kiasi gani unavaaje, unatembeaje, unasemaje, mahusiano mbele za watu.
Nyumba ya bwana ni mahali patakatifu. Musa aliambiwa vua viatu mahali hapa ni patatifu. Iweni safi mwilini na rohoni.

                  KWA NINI TUNATEMBEA KATIKA MATESO

Tujiulize mimi na wewe kwanin kwa nini tunatembea katika mateso. Ni kwa sababu ya makosa yetu, makosa waliofanya wazazi wetu, makosa waliofanya ndugu wa familia moja niliozaliwa nao,jamaa zangu wanaonizunguka au ya ukoo ninaotoka.
 Na ukisha jichunguza kote huko unatakiwa utafakari  ni kwa sababu ya kumemwacha Mungu na kutegemea nguvu zetu wenyewe ana tuna miungu mingine ambayo tunaiabudu.i
Hii yote inatoka na kujiona kuwa Mungu huyu tuliyemzoea naweza nikamuomba kitu fulani leo, kesho akanipa tu, lakini nikisha ona kila siku ninapomuomba Mungu anatenda basi hujifanyia kuwa ni mazoea. Lakini tuelewe ya kuwa Mungu wetu hazoeleki hata kidogo, ni mpya kila iitwapo leo.   
Yeremia 4:22 Wapumbavu, waliopungukiwa na akili. Mungu wetu hana iyana ametupa maarifa tele lakini kwa maarifa tulionayo tuna viburi vya kwa kumjaribu Mungu. Mwanadamu hataki akutane na majaribu yeyote yale huta njia ya mteremko tu na pindi apatapo majaribu huanza kuhoji mbona napitishwa kwenye majaribu yote haya, na kuhoji kuwa je, Mungu wewe upo.  
Watu wengi hujiuliza pia kwanini napitishwa kwenye majaribu hote haya wakati wale wa shetani wapatwi na mateso au majaribu makubwa. Lakini kaa ukijua kubwa umeshasema watu wa shetani pale hawapatwi na majaribu kwa sababu pale kwa shetani ndipo wako nyumbani kwao. Nikuulize wewe uko nyumbani itawezekanaje mgeni aje akufanyie fujo nyumbani kwako, hivyo ndivyo walivyo watu walioko kwa shetani ni wako nyumbani kwao.
 Majaribu yanaweza kutupata kutokana na kutojua au kukaidi sheria za Mungu. Hivi vyote tunatakiwa ujitafakiari kuwa wewe unazifuata sheria hizo au unaendelea kufuata utaratibu au sheria yako uliouzoea tangu hapo awali?
Kumbukumbu Torati 11:13 ikiwa wewe ni mtoto pindi mzazi wako akakuonya kwa matenda yako ambayo hayampendezi lakini wewe ukaendelea kukaidi yale maonyo unayopewa na wazazi wako. Mwisho wa yote mzazi huchoka kwa ukaidi wako hivyo huacha ulimwengu ukufunze hapo pia unawafukuza wake malaika walizi wanaokulinda ili usianguke, matokeo yake unabaki kopo tupu. Tukumbuke kuna methali isemayo‘asiyefuzwa na wazazi hufunzwa na ulimwengu’.
Kumbuka kuwa ukienda kinyume na mapenzi ya Mungu naye atakuacha, ndipo hapo shetani hupata nafasi ya kukumiliki kuanzia rohoni hadi mwilini. Maana shetani huanza kukuharibu rohoni hapo ukishaharibika matokeo ya kuharibika kwako huonekana mwilini ambapo yeye ameshamaliza kazi zake zote hufurahia ushindi huo kwa kukufanya kuwa fungu lake.
Kuna baadhi ya wanadamu akisifuwa tu kuwa yeye ni mzuri idara zote basi hapo huanza majivuno, jeuri, uzinzi wa kujionyesha kuwa yeye ni tofauti na wengine kumbe katika Yeremia 4:31 anatuonya kwa kuto kudanganyika na sifa ambazo wanadamu wenzetu nazotupa. Kwani sifa hizo wengine wanatoa sifa kwa sababu ya maslahi yao binafsi.  Uwe makini kwa kila akupaye sifa kwani wengine ni wakala wa shetani hutafuta mbinu za  kukuangusha.
Kila iitwapo leo unaenda mbele za bwana kuungama dhambi zako au unajihesabia haki muda wote, njia zako ni nyingi unawaendea wageni ambao ni miungu ambayo iliyoko chini ya miti mikubwa, majabali, mapango, baharini, njia panda, kwenye mito na hata vijito huko kote huko ulienda kupata ya ziada kuliko Mungu anayokupa. Yeremia 2:13 Uovu huu wa kumwacha Mungu, unasababisha mabirika yetu kuvuja.
Inawezekana kuwa kuna mahali hatupo sawa kimawazo, kimaneno na kivitendo na Mungu, ihali tunadai kupokea kutoka kwake. Wakati mwingine tunaenda mbele za Mungu huku mabirika yetu yanavuja kwa kujua au kutokujua, hii yote ni kutokana na mioyo yetu na roho zetu ziko mbali na Mungu. Hofu ya Mungu hatunayo tena tunaenenda kwa akili zetu tu bila kujua kuwa tunakoonda tunaenda kutumbukia shimoni.
Pindi unapovushwa kwenye majaribu ukapita salama kumbuka kuwa Mungu alikuwa nawe wakati wote huo. Hivyo usisahau kumpa Mungu shukrani kwa yote anayokutendea na hapa yule ambaye hajawaji  kupitishwa katika majaribu vivyo  hivyo unatakiwa uje mbele za Bwana kwa shukurani kwa sadaka, zaka na dhabihu ili mpate kuinuliwa zaidi ya hapo pia usisahau kumtolea Mungu nadhiri zako zote kwa maana unapojiungamanisha na Mungu ndipo mahali pako salama unapojichagulia katika ulimwengu huu.  Kumbukumbu la Torati 12:11
Umejilindaje na choyo,  hapo Luka Mtakatifu anataka ujitafakari wewe kama wewe katika ulimwengu huu uliojaa anasa na machukizo mbele za Mungu. Luka 12:15 anasema, Tujilinde na choyo  maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyonavyo.  Tutafute heri kwa kumtolea Mungu
Wakorinto 2: 4-16 Utu wa nje unachokaa lakini utu wa ndani unatakiwa uwe na nguvu pia uwe imara na hata kama utakuwa unajaribiwa katika mapito yeyote yale unayopitia. Usije ukaucha utu wako wa ndani uharibike kwani unapoharibika utu wako wa ndani kwa dhiki hiyo ya nje, kumbuka usiviangalie vinavyoonekana kwani hivyo ambavyo ninaharibu utu wako wa nje, bali viangalie sana tena kwa macho mawili vile ambavyo havionekani ambavyo ni vya milele.
Maisha yako ya utaishije hapa duniani umejiuliza wewe mwenyewe au umemshirikisha Muumba wako. Je kwa akili zako unaweza kuishi hapa duniani bila maada wowote utokao kwa Mungu?
Lakini Isaya 45:11 anakujibu swali hilo na kusema, Bwana Mtakatifu wa Israeli Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari za kazi ya mikono yangu; haya! Niaagizeni. Je, umemuuliza vingapi katika maisha yako, watoto, ndugu, jamaa na marafiki wanakuzunguka? Na kama ulisha muuliza je umemuagiza akufanyie nini hapa duniani?
Kumbuka kuwa kama kila ufanyalo haliendi na kila utendalo halifanikiwi unapaswa umshirikishe Muumba wako ndiye yeye ajuaye yote yajayo na yakupatayo kwenye maisha yako na familia yako, kazini, kwenye biashara zako na hata kwenye kazi zozote zile ambazo si kinyume na yeye na umuagize unataka nini akufanyie. Kumbuka kuwa si kwa mapenzi yetu bali kwa mapenzi yake yatimizwe.


                                                  KUKOMBOA UZAO
Katika maisha ya kila mwanadamu lazima kila mtu amezaliwa na wazazi wote wawili. Asiye zaliwa na wazazi wote wawili nia Adamu na Eva tu. Lakini kizazi kilichofuatia baada ya hapo wote wana wazazi wawili.
Kuna aina nyingi za uzao, lakini leo tuangalie uzao wa damu. 1 Petro:1:23, anasema kuwa tumezaliwa mara ya pili, si kwa mbegu inayoharibika. Lakini mtoto anapozaliwa kumbuka kuwa shetani huko mlangoni akisubiri akitafuta kile ambacho mtoto anapozaliwa na kitu chake cha Kiungu akiharibu wakati ule ule.
Mtoto hana tofauti na mtumwa Wagalatia 4:1. Mtoto anapozaliwa huwa mzazi au mlezi wake ndiye anayekuwa kiongozi wake kwa kila kitu hadi hao atakapokuwa na fahamu zake za kuweza kujitegemea mwenyewe.
Mwivi haji ila kuiba na kuharibu na hata kuchinja Yohana 10:10, kumbuka kuwa mwizi yeyote anayeenda kuiba haendi pale kwa kutoa taarifa kuwa anakuja kuiba, wewe hushitukia tu kuwa ameshakuja kuiba. Sasa shetani ndiye mwivi wetu wa vile ambavyo Mungu ametupa sisi tangu kabla hatujaumbwa na hata tukiwa tumboni mwa mama zetu na maisha yetu yote.
Mtoto yeyote anajifunza kutokana na kujifunza, kuona na hata kusikia kutokana na wazazi wake wote wawili. Pindi mtoto anapokuwa tumboni na baba na mama wakawa na ugomvi yule mtoto ulieko kule tumboni naye hushiriki kwa namna moja au nyingine ugomvi ule kwa njia ya kusikia.
Watu wengi husema kuwa mama akiwa mjamzito ni chanzo cha magomvi kati ya baba na mama. La hasha hii inatokana tu na wewe kutokumshirikisha Muumba wako tangu siku ile ya kwanza ulipopata ujauzito huko. Kumbuka pindi upatapo ujauzito mshirikishe Muumba wako kwa kila kitu maana mwili huo si wako peke yako ni wa Mungu pia.
Usipo mshirikisha Mungu tangu kipindi chako cha kwanza upatapo ujauzito wako kumbuka kuna mharibifu ambaye anasubiri wewe ulime shamba hilo yeye anasubiri unapoenda kulala apande magugu. Je, wewe kuna ambaye amepanda magugu kwenye uzao wako?
Pindi mtoto anapozaliwa na kukua, kasha ghafla akabadilka tabia yake, msije mkafarakana baba na mama kwa ajili ya mtoto huyo rudini nyuma huku mkitafakari kuwa je ni wapi tulipokosea tukamrudia Mungu. Je, ujauzito ulipotokea tuliukabidhi mbele za Bwana au tuliona hapa tulitengeneza sisi wenyewe? Fungua mafundo hayo ambayo yamempata mtoto mpaka anakuwa na tabia ambazo hakuna hata mzazi hata mzazi mmoja wenu aliyekuwa nazo.
Uzao wa tumbo lako ni thawabu Zaburi 127:3. Usilaumu uzao wako hata siku moja. Wewe kama mzazi unatakiwa usimame kwenye nafasi yako kama mzazi. Nguvu uliyonayo inamfuata mtoto popote pale alipo kwa wewe kusimama na Bwana. Tumia mamlaka uliyonayo kama mzazi ambaye ni Mungu wa hapa duniani.
Mtoto ni mbegu ambayo hupandwa kwenye tumbo la mama na kisha hupatikana kuwa ni mche anapozaliwa. Na akisha kuwa mtoto huyo hutoa matunda ambayo katika familia huleta furaha na upendo katika familia.
Kuna vitu vinavyoharibu uzao. Moja ya vitu hivyo ni maagano. Naomba nikuulize wewe mzazi ulishawahi kufanya maagano yeyote yake kabla ya kumpata huyo mtoto na baada ya kumpata huyo mtoto umetimiza hayo maagano?
Kuna maagano mengine ni mazuri na maagano mengine ni mabaya, kati ya haya mawili wewe ulifunga agano lipi, baya au zuri. Na kama lifanya maagano ya kumtolea Mungu kila upatapo kumbuka kumrithisha mtoto wako maagano hayo. Mfano, mzazi anaweza kuwa ni mtoaji mzuri sana na akabarikiwa kupata mali nyingi. Lakini akifa mali zote zikaenda nae. Hapo anakuwa hajawarithisha watoto wake lile agano alilolifanya na Mungu.
Angano linguine ni lile baya. Maagano haya utokana na mzazi kutafuta mtoto kwa njia isiyompendeza Mungu. Inawezekana mtoto uliyenaye umempaka kwa njia za wagaga na matambiko au hata njia nyingine unazozijua wewe.
Ukaambiwa kuwa ukitaka kupata ujauzito lazima uzini juu ya kaburi, au unapooja kaburi limechimbwa wewe nenda kachukue mzizi kule ndani ya kaburi, kwa tamaa yako ya kupata mtoto ili ndoa yako isiharibike ukafanya masharti yote hayo uliyopewa na mganga. Ukenda ukafanyiwa dawa ukapata ujauzito.
Kumbuka kuwa mzizi wowote una nguvu na kaburi nalo lina nguvu hapo utakuwa umemrithisha mtoto maagano ya kuzimu. Na hata maisha yake yote yatakuwa ni ya mateso matupu. Kumbuka shetani ni muharibifu wakati wote.
Ni nani awezae kutoa kitu kisafi kitoke kwenye kwenye kitu kichafu ni Mungu peke yake. Yeye huweza kumtoa mtu aliyepotea katika uchawi, ulevi, wizi, uasherati na vitu vingine vingi.
Usije ukafa na deni kabla ya Yesu kurudi tena mara ya pili. Kumbuka kufufua zile huduma ambazo zimekufa kwenye nafsi yako kwa kumshirikisha  Roho Mtakatifu.
Watu wanaweza kupatwa na madhara ya kupighwa kutokana na mzazi kuchukiana na mtoto. Malaki 4:5,6 inatuonya kuwa ugomvi kati ya baba na mtoto ataipiga dunia kwa laana. Umuonapo jirani yako wana ugomvi na mtoto wake kuwa moja wao wa kusuluhisha ugomvi huo kama ikishindikana wewe ingia magotini umwambie Mungu aingilie kati ugomvi wao huo.
Wazazi wasiwe vyanzo vya kuwatawanya watoto wao , hata kama mzazi mmoja wapo ana mtoto nje ya ndoa ni heri ukamharifu mwenzako kuwa una mtoto nje kuliko kungojea siku unataka kukata roho ndipo unamwambia. Hivyo utakuwa unajitesa wewe mwenyewe na utaondoka na mzigo wako.

                                               KUMTUMIKIA MUNGU

Mungu alimuumba mwanadamu kwa thamani kubwa sana, alimpa akli yenye ugunduzi ndani yake. Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyewe, lakini shetani yeye ni kiumbe kama malaika wengine.
Maisha anayoishi shetani ni ya sehemu moja nayo ni kuzimu. Na akitaka kumdhuru mwanadamu yeyete humtumia mwanadamu kumuharibu au kumdhuru mwanadamu mwenzie. Yeye shetani hana uwezo wa kumwingia mtu moja kwa moja.
Unachotakiwa kufanya ili kumuepuka huyo shetani, wewe mwanadamu ili shetani asipata mlango wa kukuingia unatakiwa uishi katika viwango vya uungu.
Bwana amekuweka kwenye bustani yake hapa dunia ili uweze kuilima na kuitunza. Mwanzo 2:15 ikiwe wewe umepewa bustani ulilime na uitunze je, hadi hivi sasa umeilima hiyo bustani na Mungu na kuitunza mazao yake. Kama umeilima je unakesha kuituza. Maana shetani yuko wakati wote akizunguka zunguka ili apande magugu ndani yake. Kumbuka kuwa macho wakati wote ukikesha kwa kuomba.
Kumbuka neno lako ni sheria malangoni pa adui. Usimuwekee Mungu mashaka unachotakiwa kufanya ni kutii na kumuamini. Wengi wa watu wanamuwekea Mungu mashaka ikiwa maombi yao yanachelewa kujibiwa kwa wakati ule aliyoomba.
Mungu wetu si kigeugeu humpa mtu kile anachostahili na si atakacho yeye mwanadamu. Na humpa kwa muda na wakati ufaao. Unaweza ukaomba uwe tajiri lakini Mungu akakupa kwanza elimu. Hiyo elimu ukiitumia vizuri ndipo kitakuwa chanzo chao cha utajiri.
Unachotakiwa kuzingatia ni Yohana 12:24, chembe ya ngano isipoanguka ikafa haitoi mazao. Vivyo hivyo mtu asipokufa katika Mungu hawezi kuwa mtumishi wa Mungu. Kubali kufa ili mbegu itakayozaliwa kwako iwe mbegu zuri na ya mfano mbele za watu.
Mungu ametutupa katika nchi sisi kama mbegu ili atuinue upya katika yeye. Ufanyapo kazi yoyote kwa elimu uliyokuwa nayo kwa upendo wa Mungu hakika, Mungu huyo huyo atakuinua. Bali ufanyapo kazi kwa matakwa yako wewe mwenyewe hakika hutafika mbali na mwisho wa yote utakuwa ni majuto, maana hapo umempa nafasi shetani afanye kazi na wewe bila ya wewe kugundua kuwa umempa nafasi hiyo shetani.
Unapoambia kwenye ulimwengu wa roho kitu fulani umpe mtu fulani, basi usifanye mashaka ya kutoa kitu hicho ulicho nacho kumpatia mtu uliyeambia na hata kama kitu hicho ndio umetoka kukinunua dukani au umeletewa zawadi. Pia elimu uliyokuwa nayo usiwe mchoyo kwa kuwasaidia wengine kwani ufanyapo hivyo utakuwa unamtangaza Mungu kwa elimu uliyo kuwa nayo.
Ili uwe na amini moyoni mwako unatakiwa utumike na Mungu. Wekeza katika Mungu hapo hakuna hata yule kibaka, shetani, mzimu, majini, vibwengo, vinyamkera, mchawi,  ambaye anaweza kuiba ambavyo umeviwekeza kwa Mungu.  
Chochote unachokipanda kwa ajili ya Mungu hutangulia kukuandalia mazingira. Kati ya Mungu na shetani wewe unamtumikia nani? Matendo ya Mitume 19:13 mtu alikuwa anatolewa pepo, lakini wakati akitolewa yule pepo akamwambia yule mtoa pepo kuwa Yesu wanamjua na Paulo wanamjua lakini wewe unayetutoa ni nani?  Usije ukamwambia mwenzio mdhambi kumbe wewe ni mdhambi zaidi yak wake.
Iwapo Samweli alimtumikia Bwana mbele ya Elia. Je wewe unamtumikia nani mbele ya nani? Au unajitumikia wewe mbele ya nafsi yako na Mungu umemuweka kando? Lazima umtumikia mtu mbele ya Bwana. 1 Samweli 3:1
Katika utumishi huo huo Joshua alikuwa mtumishi wa Musa. Pia Elisha alitumika kwa Elia. Hapo utaona manabii wa zamani wakuwa watumishi wa watu ndipo wakaja kuwa wakuu baadaye. Usipokubali kutumika sasa hutaweza kuwa mkuu.
Heshima siku zote hauwezi ukaileta wewe kwa elimu, ujuzi, akili au maarifa uliyokuwa nayo. Heshima siku zote hujitetea yenyewe 1 Samweli 3:21.
Iwapo unataka kuwa mtumishi katika hema ya Bwana lazima mtafute mtumishi ambaye yuko zaidi rohoni na sio mwilini. Ili aweze kukujenga kiroho na kiimani zaidi. Tumika mbele ya wachungaji, manabii, wainjilisti ili upate upako wao nawe uweze kufikia kile kiwango wambacho ulikuwa unatamani uwe nacho. 2 Nyakati 26:5 aliyemtafuta Bwana siku ya maono atampata.
Kwa hiyo usikate tamaa kwa njia unazopitia za kumtafuta Kristo. Wewe ukishindwa ungia magotini umuulize kuwa mimi hapa nakwama nifanye nini? Usiitegemee nafsi yako kufanya jambo ambalo liko nje ya uwezo wako.


                                       KUFUTA MASHTAKA YA KIZAZI


Usipotaka usiku huta weza kupata siku ya pili. Usipo kubali kuwa na usiku katika maisha yako ya kawaida hapa duniani huwezi kupata siku ya pili. Hapa ina maana unapopatwa na majaribu katika maisha yako lazima kuwe na mlango wa kutokea.
Kila mfanyabiashara lazima atumie mtaji ili faida ipatikane. Na asipotumia mtaji hutafahamu katika biashara yako kuwa umepata faida au hasara. Katika maisha yako lazima unapofanya kazi lazima faida yake ionekane ndipo ungundue kuwa kazi ninayoifanya ina faida kwangu.
Pindi mtu apatapo matatizo katika maisha yake ya kila siku lazima utataka kumjua Mungu kilazima, ikiwa wawe ni mtoto  wa Mungu. Matatizo katika maisha yanapokuwa katika kiwango cha juu, hapo ndipo juhudi ya kumtafuta Mungu huongezeka zaidi ya ile mara ya kwanza ulipoliona tatizo ukadhani kuwa litaisha muda si mrefu. Kumbe ndio siku inavyoziku kupita ndivyo machungu ya tatizo yanazidi afadhali na jana.
Majaribu yeyote yanayoletwa na Mungu lazima kuna mlango wa kutokea, 1  Wakorintho 10:13. Unapopatwa na matatizo lazima uwe na ustahimilivu, uwe na uwezo wa kuvumilia hiyo tatizo au matatizo hayo. Usiyumbeyumbe kwani hapo ndipo ukijisahau tu kidogo ndipo unampa shetani mlango wa kuingilia.
Umeshawahi kujichunguza kuwa wewe ni kizazi gani na kinatoka wapi? Jitafakari katika maisha yako kuwa wewe u kizazi gani cha nyoka au cha Mungu. Kizazi chako kiko sahihi au kimeuzwa kutoka na mila na destruri tuliorithi kutoka kwa wazazi  au walezi wetu.
Kwa karne ya siku hizi za teknolojia kuwa vizazi vingi watu wameviuza wenyewe kutokana na kutaka maisha rahisi na ya kifahari. Ukitaka kumfuta Mungu siku zote lazima ukutane na majaribu mengi. Njia ya kumuendea ni nyembamba huwa na milima na mabonde hakuna tambarare.
Ikiwa umeshawahi kukutana na muwindaji ukamuuliza jinsi anavyowinda atakueleza kuwa lazima uwe ni mtu jasiri. Maana ukiwa jasirisi hata ukikutana na mnyama mkali kama samba akikuona wewe u jasiri lazima atakimbia atajua hapa leo sipati kitu. Lakini ukiwa legelege kwa sekunde tu umeshakuwa kitoweo chake kizuri.
Mara nyingi shetani hutumia mbinu ya kupandikiza hofu kwa mwanadamu na hofu hiyo ikisha kuwa na mizizi ndipo udhaifu unapo jengeka. Na ukisha jengeka huanza kuwa mnyonge. Hii yote shetani hutumia mbinu ya kupandikiza sumu ya maneno.  Maneno huweza kuleta madhata makubwa katika maisha yeyote ya binadamu.
Mfano mgonjwa anapoenda hospitalini na kukutana na tabibu na yule tabibu akamuambia kuwa, kwa ugonjwa huu ulionao sikua kama utapona hapo ametumia maneno kumuambia mtu. Na yale maneno yanapopata nguvu kutoka na kujirudia rudia akilini hujenga hofu na ile hofu humuongezea mtu ugonjwa ule mara mbili zaidi hapo ndipo unaweza ukafa haraka kutoka na hofu ulioyokuwa nayo kutokana na maneno uliyoambiwa na tabibu yule.
Ikiwa katika familia kuwa mtu ana utumishi ndani yake lazima shetani hutumia mbinu wakati akiwa mdogo kuharibu utumishi wake huwa kabla haujachipuka mizizi ya utumishi. Humtafuta kizazi kile kikiwa bado kidogo hukizonga zonga kwa magonjwa hata kila aina ya matatizo ambayo mtu mwenye roho nyepesi anaweza akaanguka mwenye mikono ya ibilisi kwa kutafuta msaada wa haraka kuliko kuvumilia kwa kumwomba Mungu.
Naye Kutoka 21:1 anasema, atawapatiliza maovu ya baba zenu kutoka kizazi hadi kizazi. Hapa kinaongelewa vizazi vinne. Toka babu, baba, mtoto na mjukuu. Kizazi ndio mara nyingi shetani hukishitaki. Kumbuka Musa alipozaliwa alitaka kuuwawa lakini kwa neema za Mungu alihifadhiwa kati kati ya maadui. Je, wewe umehifadhiwa katikati ya maadui zako au hujifahamu kuwa wewe umehifadhiwa katikati ya maadui zako?
Ukiwa unajiona kuwa matatizo yako hayaishi siku hadi siku umetubu hadi umesahau ulichokuwa unatubu mbele za Mungu. Kumbuka kuwa kizazi chako ni cha Injili. Umezaa mfalme, nabii, mwinjilisti, shemasi, na vipawa vingine vingi ambavyo siku zote huwindwa na maadui pande zote ili wakiangamize kizazi hicho.
Iwapo wazazi wako walitenda dhambi nasi pia tumebeba uovu wao Maombolezo 5:7. Iwapo baba au mama yako alishiriki kwa namna mmoja au nyingine kutenda uovu wa aina yeyote ile, haijalishi alitenda wakati gani iwe kwenye mchana au usiku. Na hata wakati mwingine mzazi huyo alitenda uovu huo kwa siri, ujue kuwa lazima uovu ule utakipatiliza kizazi chake, yeye anaweza asione madhara kwa uovu ule alioutenda lakini anakipa shida kizazi chake kwa kubeba uovu wake.
Kumbuka kuwa kizazi kina malango yake, mbingu yake, nchi yake,mbawa zake. Pia kina uweza wa kuficha wengine.  Kila mbingu ina ardhi yake, kila nchi ina mazao yake ambayo huvunwa humo. Kila kitu kilichokuwa na mabawa lazima huwa na uwezo wa kuruka.
Ee mtu wa Mungu lazima uwaambie watu ukweli hata kama utachukiwa kwa sababu ya ukweli huo. Usikisahau pia kizazi chako kukiambia ukweli maana unapouhubiri ukweli ndipo uhuru kufunguliwa kutokana na minyororo ya shetani unapopatikana kwenye maisha ya kizazi chako.
Mara nyingi shetani huishitaki ndoa. Ndoa yeyote hushitakiwa na shetani kutokana na mmoja kati yao akienda kinyume na mapenzi ya Mungu  kwa uzinzi, magomvi, uchawi, na vitu vingine vingi basi hapo ndipo ummpa shetani kibali cha kukushitaki.
Ndipo hapo mtoto anayezaliwa huambukizwa fangasi hizo za magomvi, uzinzi, uchawi, matusi na mengine mengi. Mtoto hurithi tabia zote hizo ambazo wazazi walizomsababishia na humpekelea mtoto kuwa na nembo ya uchungu moyoni wakati wote.
Tukumbuke Ayubu alikuwa mtu mcha Mungu sana na alibarikiwa kwa kila kitu ikiwa ni kwa mali, watoto na vitu vingine vingi ambayo ni ndoa, mifugo, watoto, mali na vitu vingine vingi alibarikiwa navyo. Lakini shetani kwa hila zake aliona kuwa Ayubu alimcha Mungu kwa sababu amebarikiwa kwa mali zake. Akamuomba Mungu ruhusa ili amjaribu Ayubu kama kweli anamcha Mungu kwa kila kitu.
Kumbuka Ayubu alipojaribiwa wakati wote alikuwa bado anampenda Mungu kwa kila mapito aliyokuwa anapitishwa na shetani bila ya yeye kujua. Ayoubu 2:3 inasema, ijapokuwa shetani alinichochea pasipokuwa na sababu lakini Ayubu alizidi kumpenda Mungu.
Je wewe mapito hayo unayopitia unakuwa bado uko na Mungu au unakata tamaa kwa mapito hayo. Kumbuka kung’ang’ania ndio mtaji wa kumpendeza Mungu ajue kuwa kwa mapito anayopitia mwanangu huyu kweli ananipenda. Hapo lazima Mungu atakuheshimisha kwa yote.
Kitabu cha Danieli 6:1, lakini tuuangalie mstari ule wa nne (4) unasema, maliwali, madiwani, mawaziri na viongozi wote katika ufalme ule walimchukia Danieli kwa sababu ya msimamo wako wa kuwa mtu mwenye haki na mkweli mbele ya bosi wake na mbele za Mungu. Wakaamua wamuundie sheria ambayo iwapo ataikiuka basi ndipo itakuwa mwisho wa yeye kuwepo katika uongozi ule.
Lakini Danieli kwa uaminifu wake kwa Mungu hatutetereka yeye alikaza buti na aliendelea kumtukuza Mungu kwa kelele kubwa ambazo hazikuwa za siri tena. Ndipo walipo mshitaki kwa sheria yako na akatupwa kwenye tundu la simba. Lakini kwa upendo wa Mungu aliokuwa nao kwa Danieli hakuliwa na wale wanyama walikuwa ni marafiki zake. Ndipo yule mfalme aliwaamuru wale wote walioleta fitina kwake kuhusu Danieli, wachukuliwe wao na familia zao zitupwe kwenye lile tundu la simba, na kabla hawajafika chini waliraluliwa vipande vipande na kizazi chao kiliishia hapo.
Je, maadui zako wanataka wamekuandalia mashitaka ya aina gani mbele ya wakubwa wako, ukiwa kazini, nyumbani, kwenye shughuli zako zozote zile ambazo unajiendeleza nazo. Kumbuka iwapo unafahamu kuwa kuna watu wamepekela mashitaka kwa wakuu wako wewe usihofu hata kidogo kwani kuna mtetezi wako ambaye ni Mkuu kuliko wote nenda mbele zake ukamwambie hao washitaki wako naye atawashughulikia.
Ili mashitaka uliyoshitakiwa na shetani mbele za Mungu yaondolewe unafanyaje? Kumbuka kuwa wewe ni mwenye dhambi lakini dhambi hiyo imesamehewa kwa Damu ya Yesu pale msalabani. Kwa hiyo usije ukajihesabia dhambi wakati ulisha samehewa.
Kumbuka kuwa kila aliye dhaifu na aseme yeye ni hodari Yoeli 3:10. Iwapo mtu yeyete atakutamkia kitu kibaya wakati huo huo wewe kanusha kwa kusema kinyume chake, mgongwa sema mimi ni mwenye afya. Ukiambiwa kuwa wewe ni masikini wewe sema mimi ni tajiri mbele za Bwana.       
  








                                                                                  






                                                    



                                                                            
                                                                 

No comments:

Post a Comment